Thursday, December 22, 2011

ELIMU TANZANIA


Nawapa pongezi wale wote wenye moyo wa kuendeleza elimu nchini. Elimu ndio msingi wa maendeleo katika nchi yoyote. Ikiwa elimu itapewa kipaumbele na kuthaminiwa basi itakuwa kweli msingi wa maendeleo. Elimu ikiwa ni kitu cha kudharauliwa itakua ni msingi mbovu sana wa maendeleo ya taifa husika. Taifa linalodharau elimu ni taifa potovu na lina mwisho mbaya.

Elimu bora inajenga taifa la watu wenye utambuzi na ufikiri mzuri. Elimu bora inajenga watu wenye maamuzi mazuri katika maendeleo ya nchi yao. Elimu ndio chanzo kizuri cha usimamizi wa ushirikiano kati ya jamii moja hadi nyingine kwani katika elimu imejaa busara na hekima. Elimu bora ikitumiwa vizuri ni kitu kizuri sana kwa maendeleo ya nchi na ikitumiwa vibaya ni sumu kari sana isiyo faa duniani.

Elimu isiyo bora si kitu cha mnufaa kwa mtu wala taifa lake. Elimu pasipo matumizi mazuri ya elimu hiyo ni ujinga na wala hauitajiki katika dunia ya kisasa. Elimu dhahania haifikishi popote taifa husika. Elimu isiyo bora inajenga taifa la watu wasio staarabika.

Kwa siku za hivi karibuni waajiri wamekuwa wakilalamikia uwezo wa wanafunzi watokao vyuo vikuu kwamba hawana uwezo mzuri wa kutenda kimatendo yale waliyosomea vyuoni. Siwashangai waajiri wala siwashangai wanazuoni kwa kukosa uwezo mzuri wakiutendaji. Waajiri wanalalamikia kitu ambacho kiko dhahiri na ni haki yao kufanya hivyo na wanazuoni wanahaki yakutojua vyema nini wanatakiwa kufanya katika ulimwengu wa matendo. Waajiri wanapenda kupata mtu atakaye zalisha na asiwe mzigo kwao. Wanazuoni nao wanapenda kuwa hivyo lakini kuna mambo mengi yanayo sababisha wakose ujuzi na mbinu za utendaji kimatendo. Mtoto wa kitanzania, mtoto anaye anza darasa la kwanza hadi kumaliza shahada yake nchini anakabiliwa na mambo magumu katika safari yake ya elimu. Safari inayohitaji uvumilivu mkuu na inayohitaji kujituma sana ili kuifanikisha.

Elimu ya Tanzania ni bora elimu kutokana na sababu nyingi. Lakini sababu ishirini nitakazo zielezea moja baada ya nyingine ni vyanzo vikuu vya elimu ya Tanzania kutokuwa bora.

Sababu zinazo kwamisha ubora wa elimu nchini ni kama ifuatavyo;

1. Walimu wote nchini wanafaa kuwa walimu? Walimu wanapatikana kwa namna ipi? Nini kinamfaa mtu kuitwa mwalimu? Ni maswali matatu kati ya mengi ya kujiuliza kuhusu mwalimu na yanaleta majibu tofauti sana. Wengi wa walimu wetu nchini katika ngazi zote za elimu hawafai kuwa walimu. Wengi wamekimbilia katika fani ya ualimu baada ya kuanguka katika masomo yao. Je! Nitawezaje mfundisha mtu kitu ambacho mimi kilinishinda? Mtu akifanikiwa kuingia chuo cha ualimu basi mtu huyu ameshakuwa mwalimu hata kama atasoma kwa mbinu za udanganyifu lakini akafanikiwa fauru mitihani yake basi ni mwalimu ambaye serikali itajivunia. Si haba mwalimu huyu kufika na kuandika ubaoni pasi kutoa maelezo yeyote na kuwambia wanfunzi wasome vitabu wataelewa. Kwa vyuo vikuu, mtu kupata alama za juu anafaa kabisa kuwa mwalimu na wala hajalishi mtu huyu amezipata kwa mbinu zipi. Mwalimu ni mtu mwenye uelewa katika yeye, anayejiamini na mwenye uwezo wa kutoa taaluma anayo ielewa kwa wengine bila uoga wala kusita. Kama mwalimu atakuwa hivyo basi elimu atakayo wapa wanafunzi wake itakuwa ni elimu ya kuvutia na yenye manufaa vinginevyo wanafunzi nchini watakuwa ni watu wa kukariri daima.

2. Wizi wa mitihani si kitu kigeni masikioni mwa watanzania wengi na ifikapo wakati wa mitihani wanafunzi uzunguka huku na kule kutafuta mitihani. Kuwa na taifa la watu wezi kwa namna hii si kitu cha ajabu. Kuwa na taifa la watu wasio jiamini si kitu cha kushangaza na kuwa na taifa la watu wanaojua kukariri ni kitu cha kawaida katika hili. Wizi wa mitihani sasa nchini unafanywa ngazi zote za elimu. Mara nyingi tumesikia wizi wa mitihani umetokea, mwaka 1998 wahitimu wa kidato cha nne walilazimika kurudia mtihani kwa uvujaji mbaya wa mitihani, mara nyingi tumesikia walimu wamechukuliwa hatua kwa wizi wa mitihani na pia wanafunzi kufutiwa matokeo yao. Nini chanzo cha wizi wa mitihani na ni nani hasa wanaohusika katika wizi huu? Kama serikari inaweza kupeleleza na kukamata majambazi yaliyo husika katika tukio la uharifu iwaje serikali hiyo ishindwe kutambua chanzo cha wizi wa mitihani na kukiziba? Mwanafunzi imara ni Yule anayeshikilia mafundisho na kuelezea vizuri sana mafundisho hayo pale anapotakiwa kufanya hivyo.

3. Ni mara ngapi mfumo wa elimu nchini umelalamikiwa na usirekebishwe? Muhitimu wa darasa la saba ana elimu ndogo sana ya dunia na ndivyo elimu yetu ilivyo mjenga. Mtu huyu hawezi jitegemea kwa kutumia taaluma yake na wala hafai hata kuwa karani. Elimu yetu ndivyo itakavyo kwani hata cheti cha darasa la saba kimekuwa kikionekana si cha muhimu tena. Mtu wa kidato cha nne anaweza kuwa karani ila baada ya kozi Fulani na anaweza kuwa mwalimu mzuri wa shule ya msing asipokuwa na mafanikio mazuri katika masomo yake. Mtu wa kidato cha sita atafaa kuwa mwalimu wa sekondari asipokuwa na mafanikio mazuri katika masomo yake na uhitaji kozi Fulani Fulani kuwa kupata uelewa kidogo wa fani Fulani na vivyo hivyo kwa Yule aliye maliza masomo yake ya chuo kikuu kuitaji mafunzo zaidi ili kuwa na ujuzi wa taaluma yake. Wengi hawafani pasipo mafunzo ya ziada na hii inaonyesha mfumo wa elimu ya Tanzania ni wa kutoa watu ujinga na si kuwaandaa kuwa wataalam na wajuzi wala sio wa kuwaandaa wanafunzi kuwa wabunifu na wenye kujiamini. Mfumo mzuri wa kitu Fulani ndio hasa utambua mahitaji ya wakati huo na baadaye na ndio utambua nini kifanyike wakiti huo kukidhi mahitaji na nini matokeo yake kwa manufaa ya baadaye. Vivyo hivyo katika elimu, mfumo mzuri ndio hasa utatoa wakufunzi wajuzi kwa manufaa ya nchi yetu sasa na baadaye.

4. Mawasiliano kati ya mwalimu na mwanafunzi, kati ya mwalimu na kati ya jamii na mwanafunzi ni muhimu sana. Lugha imekuwa kikwazo kikubwa sana katika katika utowaji wa elimu nchini. Mabadiliko ya lugha toka shule ya msingi mwanafunzi aiapo sekondari hayafai. Mtoto ushika lugha vyema anapofundishwa na kuitumia, hivyo mwanafunzi anapotumia Kiswahili tokea darasa la kwanza ataishika na kuwa muelewa katika Kiswahili. Inapotokea lugha inabadilika ghafla wanafunzi wengi uanza maisha ya kukariri. Maisha hayo ya kukariri hayabadiriki mpaka wanapohitimu elimu ya juu. Mawasiliano mazuri kati ya mwalimu na mwanafunzi, kati ya mwalimu na jamii na kati ya mwanafunzi na jamii yanajenga vyema uhitaji na uelewa wa wataalam katika fani mbalimbali.

5. Ili mwalimu kuweza kumfundisha mwanafunzi vyema nyenzo muhimu zatakiwa. Ili mwanafunzi kuweza muelewa mwalimu vizuri nadharia kidogo na matendo mengi yanahitajika. Shule nyingi za msingi na sekondari hazina maabara na zile zenye maabara hazina vifaa vya kutosha na vinavyokidhi mahitaji ya elimu kwa mwanafunzi. Vyuo pia vivyo hivyo. Zipo shule zenye vifaa vichache na walimu wasijue jinsi ya kuvitumia. Hii hainishangazi kwani wengi wa walimu wetu inajulikana ni watu wa aina gani. Elimu ya utambuzi yahitaji vitendo zaidi kuliko nadharia. Mtoto wa kitanzania ategemea kuwa mgunduzi wakati maabara ameiona akiwa kidato cha tatu au nne, akiwa na akili iliyo komaa na inayojua elimu ni kufauru mitihani kwa kukariri tu!

6. Mtaala ni muongozo mzuri wa elimu kwa walimu na wanafunzi pia. Kubadilibadili mtaala ni sawa na kuchimbachimba barabara ili watu walio mbele wapate taabu ya kurudi na kuwaelekeza njia wale walio nyuma na pia wale walio nyuma wapate taabu ya kusonga mbele. Walimu na wanafunzi wamekuwa wakipata taabu sana kwa mabadiliko ya mara kwa mara ya mitaala ya elimu. Mwalimu mkufunzi wa fizikia anapata taabu ya kufundisha somo la sayansi lenye muunganiko wa fizikia na kemia. Masomo hayo yanatofautina, hitoria yake yajielezea katika kutofautisha masomo hayo. Kuunganisha masomo bila kutambua historia zake ni sawa na kubumba dunia yetu ya dhaania.

7. Kusoma masomo ya sayansi au ya historia ni vyema. Mwanafunzi katika ngumi pekee ana uhari wa kufanikiwa zaidi ya mwanafunzi anayefumbata ngumi pamoja na jiwe. Mgawanyo wa masomo katika elimu ya awali na hasa ile ya sekondari ni muhimu sana. Mwanafunzi wa kilimo na apewe mafunzo ya kilimo zaidi na masomo ya ziada machache ili kumjenga imara katika taaluma ya kilimo. Mwanafunzi wa ufundi na wa historia pia. Mwanafunzi wa ufundi kuwa na masomo mengi ya historia ni kupoteza muelekeo. Mtu hawezi kuwa yote. Mwanafunzi hawezi kuwa mtaalam aliye bobea katika fani Fulani kwa kusoma masomo yote. Kutokuwa na mgawanyo imara wa masomo kwa wanafunzi kutokana na fani mbalimbali kunawapotosha wanafunzi wengi na kuwafanya wasijiamini katika taaluma mbalimbali. Mtu wa historia kuwa mhandisi ni kumtesa mtu huyo, vivyo hivyo kwa afisa kilimo kwenda kutibu watu ni kukebehi taaluma nyingine.

8. Je! Masomo ya shule ya msingi yanafaa kufuatwa kwa muda wa miaka saba? Masomo sekondari yanafaa kufuatwa kwa miaka mine? Masomo ya kidato cha tano na cha sita yanastahili kuwa masomo ya miaka miwili? Kwamba mfumo wa elimu yetu wa 7-4-2-3/4 unafaa? Basi mgawanyo wa muda wa masomo ni jambo jema sana katika kuandaa wanataaluma mbalimbali. Mgawanyo wa miaka ya mwanafunzi kuanzia shule ya msingi mpaka chuo kikuu kama nilivyo ainisha juu kuna sehemu unatesa wanafunzi wengi na kuna sehemu muda mwingi hupotea bure. Muda ni bidhaa aghari sana, kuchezea au kushindana nao ni kujiumiza mwenyewe. Wanafunzi wengi wanakua hadi uzeeni hawaheshimu muda sababu toka utotoni walifundishwa kuwapo kwa muda wa hovyohovyo.

9. Kulia asali, kushoto mua, nile nini? Mfanya biashara aliyeishikiria biashara yake vyema awezaje kuwa mwalimu? Walimu wengi wamesahau taaluma zao na kujikita katika shughuli nyingine mbalimbali. Mwanafunzi uhasirika sana kufundishwa na mwalimu ambaye mawazo yake huwa mbali na ufundishaji. Hali ya kufundishwa na watu walioshika mambo matatu matatu kumewafanya wanafunzi wengi kuwa ni watu wa kukariri kwani wakufunzi huwa ufika na kupiga stori chache na kuacha mambo lukuki kwa wanafunzi kujisomea pasi kuelekezwa vizuri.

No comments:

afrotanza gallery