Thursday, April 14, 2011

DAMU INA RADHA TAMU

Damu kitu ni aghari sana. Hakuna hasiye tambua huwezi ishi bila damu. Damu ni muhimu kwa afya nzuri kwa kuwa mwili unategemea damu isukume oksijeni na viambatanishi vingi ili weza zifikia seli zake. Moyo hufanya kazi ya kusukuma damu lakini hauwezi ishi pasipo damu. Damu inabeba caboni dayoksaidi na taka mwili nyingine kupeleka kwenye mapafu, kibofu na kwenda kwenye mmeng'enyo wa chakula ili viweze tolewa nje ya mwili kama taka mwili. Pasipo damu tusinge weza pasha wala pooza miili yetu, tusingeweza pambana na magonjwa na wala tusingeweza toa taka mwili. Damu inathani kubwa.

Kila kitu chenye thamani mwilini au ardhini, mjini au porini, kwa mtu au mnyama uhitajika na mtu, ardhi na wanyama pia. Watu wanadamu katika miili yao na inapopungua wanaongezewa ikipatikana, wanyama pia vivyo hivyo. Ardhi haina damu kama damu ya mtu au myama lakini inapenda sana damu ya mtu au mnyama kwa kuwa damu ni tamu.

Ardhi ikionja damu haichoki kuhitaji hitaji hilo tamu. Ardhi niishiyo imeonja na sasa imezoea damu. Kwa kuwa mchovya asali hachovyi mara moja basi ni vigumu kwa ardhi ya nchi yangu kuikana damu tamu tena damu ya watu.

Msitu wa pande damu ilimwagika wazi hilo twalijua, Dito aliipa ardhi inachokitaka wazi bila kuogopa, zanzibar watu wakauana tukapata wakimbizi, wakulima na wafugaji kuilisha ardhi tamu yake kila kukicha, Arusha yakatokea ukweli mewekwa kwapani, machweo na mawio yakafika Madale ardhi kupigania damu nyingi na tamu kwa ardhi mwagika. Mtanzania mpenda amani na haki alikuwepo jana leo hapana kesho kitendawili. Watu wanajichukulia sheria mikononi kuchinja wevi na maisha yaendelea. Jazba haina utu. Chochoko ya ardhi kutaka damu haitaisha kwa kuwa imeshazoea sasa na itafitini kwa kila namna ipate tamu ya damu.

Mtanzania kupiga na kuua mtanzania mwenzake si jambo baya na wala hajutii. Anafurahi na kushaingilia na kuendelea na maisha pasi na wasi. Thamani ya maisha ya mtu mwingine kwa mtanzania wa chini na hata wa juu haipo. Waliomwaga Damu pande ni viongozi walo aminiwa na kupewa vyeo katika taifa letu na waliomwaga damu madale ni masikini kama mimi. Ardhi inataka Damu.

Kiu ya ardhi ikiwa kuu ni majuto. Pitia simulizi za vita ya Kimbali Rwanda, pitia simulizi za somalia na nchi nyingi ambazo hazikuona thamani ya mwingine katika maisha na kujiona wao ndio bora zaidi. Kabila kwa kabia, dini kwa dini, masikini kwa tajiri, tabaka kwa tabaka, ardhi haina shaka uaneni ipate shibe, inywe damu tamu ishibe.

Sintoishangaa Tanzania ya vita, kwani utu si kitu kwa raia wa tanzania. Madale watu wameuana kwa panga na marungu tena kwa kuangaliana usoni bila shaka yoyote nini kumpiga yule wa dini fulani au chama fulani?

Damu ina radha tamu. Mungu apishe mbali kiasi cha damu ardhi ya tanzania ilivyo kunywa kiwe chatosha. Awajalie watanzania utu wa kujali utu wa watu wengine, azijaze nyoyo za raia wa Tanzania ujasiri wa kuchukia sheria mikononi, watu watumie madaraka yao kwa matakwa ya wote, wakimbie rushwa, wapendane na kujua sisi wote ni ndugu, tabaka fulani na tabaka fulani, dini fulani na dini fulani Mungu wetu ni mmoja.

Damu ni tamu na ardhi inahitaji damu nyingi. Tusipojali utu tutapigana, tutauana na hakuna jema litakalo tufika.

Amani na Upendo.

No comments:

afrotanza gallery