Arnold Schwarzenegger.
Arnold Schwarzenegger leo ameachia rasmi ugavana wa jimbo la California nchini Marekani na kufanya mashabiki wake kusubiria kwa hamu kujua nini kinafuatia katika mfululizo wa maisha yake.
Baada ya miaka saba ya ugavana katika jimbo hilo, bingwa huyo wa zamani wa kunyanyua vitu vizito aliyegeuka na kuwa muigizaji mahiri wa filamu kabla ya kuingia katika siasa, Schwarzenegger anajiandaa kumuachia nafasi hiyo Jerry Brown wa chama cha Democrats.
Aidha mtaalamu huyo wa filamu amesema historia itakuwa muamuzi mkuu wa utawala wake, na kuwa anaachia ofisi akiwa na furaha kwa yale waliofanikiwa kuyatimiza chini ya uongozi wake.
Pamoja yote aliyofanya na mabadiliko ya kiuchumi katika jimbo la California, lakini macho na masikio ya wengi yanasubiri kujua wapi gavana huyo mwenye umri wa miaka 63 ataelekea baada ya kutoka katika siasa, huku wengi tukijiuliza je atarejea kwenye filamu…????
No comments:
Post a Comment